Thursday, 22 June 2017

JOIN INSTRUCTION FORM FIVE 2017



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS- TAMISEMI
SHULE YA SEKONDARI TUMAINI
S.L.P.533,
IRAMBA-SINGIDA
TAREHE, 14/06/2017
Simu:  0684534655/0762184451
Mkuu wa shule:  Honoratha J. Mbiaji.
Blog:  tumainisecondary.blogsport.com
MZAZI/MLEZI WA MWANAFUNZI……………………………………………………
S.L.P………………………………………

YAH: MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI TUMAINI HALMASHAURI YA IRAMBA MKOA WA SINGIDA.

1. Nafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika shule ya sekondari Tumaini iliyoko Wilaya ya IRAMBA katika mkoa wa SINGIDA  mwaka 2017 tahasusi ya……………………………..
Shule iko kilomita zipatazo 70 kutoka  Singida mjini kando kidogo mwa barabara itokayo Singida kwenda Mwanza. Kutoka  Singinda kuna mabasi ya SIMANJIRO,KIRUMO na HIACE ambayo huondoka Singida kati ya  saa 6:30 na saa 7:00 mchana kila siku kwenda kiomboi na hupitia Kinampanda mahali shule ilipo. Nauli ni shilingi 4,000/=. Endapo mwanao atapanda mabasi ya kutoka Tabora, Nzega, Kahama, au Mwanza kwenda Arusha au Dar es salaam ashukie sehemu iitwayo KITUSHA, kisha akodi pikipiki hadi shuleni( km.8). Akifika Kitusha  kabla ya saa 7:00 mchana asubiri Basi inayotoka singida au Kiomboi kupita Kinampanda. Shule ipo jirani na chuo cha ualimu Kinampanda.
Muhula wa masomo unaanza tarehe 02/07/2017 Hivyo mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni  kuanzia tarehe 17/07/2017. Mwisho wa kuripoti ni tarehe 31/07/2017.

2.      MAHITAJI MUHIMU YA KUZINGATIA
2.1  Sare ya sahule
a)      Sare ya shule hii ni  sketi bluu Bahari (light blue) mbili(2), mshono wa Rinda bapa(box)mbele na nyuma, Mashati mawili(2) ya mikono mirefu.
b)      Rangi ya hijab ( kijuba) ifanane na sare  ya shule,  nusu kanzu nyeupe isiyobana mwili pamoja na sketi  ndefu rangi bluu bahari.
c)      Viatu vya shule ni vyeusi vya kufunga na kamba  vyenye visigino vifupi-Jozi mbili(2)
d)     Soksi jozi tatu nyeupe za shule.
e)      Sweta bluu Bahari yenye shepu ya V  mbele.
f)       Nguo za kushindia(shamba dress)sketi nyeusi mbili,mshono marinda ya kutazamana na T-shirt mbili(2) za kuvaa nje ya darasa( aje na shilingi 20,000/=)
g)      Tai mbili(2) rangi ya  kufanana na kitambaa cha sketi, iwe fupi yenye lastiki shigoni.
2.2  Ada na michango ya shule
a)      Ada ya shule kwa mwaka ni shilingi 70,000.00 kwa mwanafunzi wa bweni, mwanafunzi anatakiwa kulipa shilingi 35,000.00 kwa muhula au kulipa ada yote kwa maramoja. Fedha hizo zilipwe kwenye Akaunti ya shule Na.5061100179(Tumaini secondary school Recurrent A/C)NMB (Tafadhali andika jina la mwanafunzi kwenye pay in slip) aje nayo anaporipoti shule.
b)     Michango inayotakiwa kulipwa na kila mzazi/mlezi.
                                                                    i.            Shilingi 15,000/=kwa ajili ya ukarabati wa samani
                                                                  ii.            Shilingi 6,000/=kwa ajili ya kitambulisho na picha
                                                                iii.            Shilingi 20,000/=kwa ajili ya taaluma
                                                                iv.            Shilingi 30,000/=kwa ajili ya kuwalipa wapishi na walinzi na vibarua wengine
                                                                  v.            Shilingi 2,000/=nembo ya shule
                                                                vi.            Shilingi 10,000/= kwa ajili ya  huduma ya kwanza   pamoja na Bima ya Afya.
                                                              vii.            shilingi 20,000/= mitihani ya kujipima mock
                                                            viii.            shilingi 5,000/=fedha ya tahadhari (haitarejeshwa)

NB: fedha za michango mingine zilipwe kwenye a/c no.50610005452-Tumaini secondary school self reliance.  Mwanafunzi aje na Bank paying slip original yenye jina lake.

2.3 Mahitaji muhimu ambayo mwanafunzi anapaswa kuleta shuleni ni:-
                        2.3.1.Vifaa vya darasani
                        (a)Madaftari makubwa 8(counter book) (b) Kalamu za wino (c) Mathematical set
                        (d)Ream A4 moja ya karatasi kwa ajili ya mitihani (e) Penseli(f) Rula
                        (g) Dictionary advanced learner
                        (h) Calculator-non programmable kwa Geography na economics
                        (j) Aje na results slip (original),picha nne  passport size za wazazi au walezi
                        wanaoweza kukutembelea shuleni.
                        2.3.2.Vifaa vya kulalia
                        (a)Godoro (sponji) futi 2.5 inch 4 (b)Net ya Mbu
                        (c)Mashuka mawili(2) light blue  (e) Mto wenye foronya light blue (f)Blanketi 1
                        2.3.3.Vifaa vya  chakula
                        (a)Sahani (b) Bakuli (c) kijiko (d) kikombe (e) chupa ya kuwekea maji ya kunywa
                        2.3.4.Vifaa vya usafi binafsi
                        (a)Ndoo 2( lita 20 na lita 10)  (b)Mswaki na dawa ya meno (c)Malapa (d)Sabuni
                        Za kufulia na kuogea.
                        (e)HKL-waje na jembe lenye mpini,HGK- Reki1 yenye mpini,HGE-Watering can
                        HGL -Panga lililonolewa,( Mifagio ya ndani( soft broom) na mifagio ya nje
                        (Chelewa) ni  kwa wote.

Wako katika ujenzi wa Taifa.
H.J.Mbiaji
MKUU WA SHULE 




SHULE YA SEKONDARI TUMAINI.
MAKOSA YANAYOWEZA KUMFUKUZISHA MWANAFUNZI SHULE

i.                    Utoro
ii.                  Wizi
iii.                Uasherati, ushoga na ulawiti , Kuoa au kuolewa.
iv.                Kupata ujauzito au kutoa mimba.
v.                  Ulevi au unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya .
vi.                Uvutaji wa sigara au bangi.
vii.              Kuharibu kwa makusudi mali ya umma.
viii.            Kupigana mwanafunzi kwa mwanafunzi,kumpiga mwalimu au na mtu yeyote Yule.
ix.                Kudharau Bendera ya Taifa
x.                  Kulala nje ya shule bila ruhusa ya Mkuu wa shule
xi.                Kutembelea majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni
xii.              Kugoma kwa namna yoyote au kuchochea vurugu
xiii.            Kutoa lugha ya matusi au lugha chafu kwa mwanafunzi,walimu,walezi,na jamii kwa ujumla.
xiv.            Kumdharau mwalimu, Kiongozi, Mfanyakazi na jamii kwa ujumla
xv.              Kutohudhuria vipindi kwa uzembe
xvi.            Kutofanya mitihani kwa makusudi/bila sababu ya msingi
xvii.          Kushirki matendo ya uhalifu, siasa na matendo yoyote yale yanayovunja sheria za nchi.
xviii.        Kufanya jaribio lolote la kujiua, au kutishia kujiua kama kunywa sumu n.k
xix.            Kumiliki simu.













FOMU A:
WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKINOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI
SHULE YA SEKONDARI TUMAINI.


FOMU YA KUKUBALI  NAFASI  ALIYOPEWA  MWANAFUNZI

A.   
Picha
Ya
mwanafunzi
 
Habari za mwanafunzi:
                                i.            Jina kamili…………………………………………………………………….
                              ii.            Tarehe ya kuzaliwa………………………..Wilaya……………………………
                            iii.            Dini……………………….Dhehebu………………………………………….
Mahali atakapokuwa anaenda likizoni:
                                i.            Jina…………………………Uhusianao……………..Mahali……………..
                              ii.            Jina…………………………Uhusiano………………Mahali……………..

Kukubali nafasi:
Mimi………………………………………nimeona maelekezo ya kujiunga na shule ya Sekondari Tumaini. Nakubali kutimiza masharti yote ya shule ikiwa ni pamoja na kutii sheria za shule. Nitakapokuwa shuleni, nitajitahidi kwa uwezo wangu wote kusoma kwa bidii na kuchapa kazi za mikono kwa bidii ili kutimiza lengo la kupata elimu katika ujumla wake.

Saini………………………..Tarehe………………………………………………………..

B.    
Picha
Ya
Mzazi/mlezi
 
Habari za Mzazi/Mlezi
                                i.            Jina kamili………………………………………………………………
                              ii.            Yeye ni mzazi au mlezi…………………………………………………
                            iii.            Uhusiano uliopo na mwanafunzi……………………………………….
                            iv.            Kazi yake………………………………………………………………
                              v.            Anwani ya kazini………………………………………………………
                            vi.            Namba ya simu………………………………………………………….
                          vii.            Anwani ya nyumbani………………………………………………………………
                        viii.            Uthibitisho wa Mzazi/Mlezi:
Nimehakikisha maelekezo na maagizo yameeleweka na mtoto wnagu atafuata sheria na taratibu zote za shule ya sekondari Tumaini.

Jina……………………………………..Saini……………………Tarehe………………



 FORM B:

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION


PART A:

TO:  The Medical Officer                                        FROM: The Headmistress,
         _______________________                                      Tumaini Sec. School,
         _______________________                                       P.O. Box 533,
         _______________________                                       Kinampanda,
                                                                                              IRAMBA – SINGIDA.
                                                                                              DATE_____________  


            NAME________________________________

Please examine the above named person as to her fitness for re-engagement as a
student in our school.


                                       Signature _________________________
                  


PART B:       MEDICAL CERTIFICATE
                      (To be completed by Medical Officer)

I have examined the above named person ad consider that she is___________
________________________________________________________­­­­­­­­______
______________________________________________________________

Date______________________   Signature __________________________

Station____________________   Designation _______________________